Waifu
wa jamaa mmoja alikuwa akisumbuliwa sana na njemba fulani iliyokuwa
ikimtaka kila siku, hatimae waif akamwambia mumewe. Mume akamwambia
mkewe, "Unajua watu kama hawa dawa yao ndogo tu,we mkubali tu, ila
mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha
ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha,
mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu".
Mamaa
akafuata masharti ya mumewe na hatimae akaweza kuirubuni njemba hadi
wakaingia chumbani, mume akawa tayari na panga uvunguni mwa kitanda
anangojea signo.
Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona njemba
ina makovu makubwa kifuani na mgongoni akaamua kuuliza, "Hee jamani
mbona una makovu hivyo?", Njemba huku ikiendelea kuvua suruali ikajibu,"
Niwe mkweli mie nina pepo la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa
wakipanga kunifumania, nimeshafumaniwamara kumi na tisa, na wote
walionifumania nimewaua". Mamaa akbaki kuduwaa tu. Jamaa alipomaliza
kuvua nguo mdada akaanza kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni,
mume kabana kimya, kila jitihada za mdada kupunga mkono hazikupata
majibu, mpaka njemba ikamaliza shughuli zake akatokomea.Ndipo mume
akatoka uvunguni jasho linamtoka,"Sasandio umefanya nini mume wangu?
Umeacha nimeshindwa kufanya lolote, kwanini hukutoka jamanii?" . Mume
akajibu kwa ukali," We we we, mwenyewe umesikia kasha ua 19 unataka niwe
wa ishirini? nauliza unataka niwe wa 20 kusudi muendelee na uasherati
wenu?